• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 17 wauawa katika mgahawa nchini Burkina Faso

    (GMT+08:00) 2017-08-14 19:24:46

    Watu 17 wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya kundi la watu wenye silaha kushambulia mgahawa unaouza chakula cha Kituruki katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou jana jioni.

    Taarifa iliyorolewa na serikali ya nchi hiyo imesema, shambulizi hilo la risasi lilitokea kwenye mgahawa ulioko mtaa wa Nkrumah majira ya saa tatu usiku kwa saa za huko. Vikosi vya usalama vilipelekwa kwenye eneo la tukio na kuweka vizuizi katika maeneo ya jirani, ambavyo bado havijaondolewa mpaka sasa.

    Uraia wa watu waliouawa mpaka sasa bado haujafahamika.

    Burkina Faso imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni, ambapo mwanzoni mwa mwaka jana, watu waliokuwa na silaha walishambulia hoteli ya kifahari ya Splendid na kusababisha vifo vya watu 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako