• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 170 wafa maji katika msimu wa sikukuu nchini Algeria

    (GMT+08:00) 2017-08-14 19:25:14

    Wizara ya ulinzi wa raia nchini Algeria imesema, zaidi ya watu 170 wamekufa maji nchini humo tangu mwanzoni mwa Julai.

    Wizara hiyo imesema, kati ya watu hao, 102 walikufa maji karibu na pwani huku wengine 70 wakifariki katika mabwawa ya kuogolea yaliyoko majumbani, na kwamba vifo hivyo vimetokea kwenye maeneo yasiyo na walinzi.

    Julai na Agosti ni msimu wa sikukuu nchini Algeria, ambapo mamilioni ya wananchi wa huko wanatumia muda wao katika pwani ya kaskazini mwa bahari ya Mediterranean ili kuepuka joto kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako