Takwimu za robo ya tatu mwaka wa fedha 2016-2017 kuanzia Januari hadi Machi 2017, ilibainisha kuwa usajili ulishuka hadi milioni 25.7 kutoka milioni 26.6 katika robo ya mwisho.
Hata hivyo, idadi ya watumiaji wa intaneti iliongezeka kwa asilimia 2.3 na inakadiriwa watumiaji wameongezeka hadi watu milioni 40.5 kutoka milioni 39.6.
Kwa upande mwingine, idadi ya usajili wa mtandao ilikua kwa asilimia 3.4 ikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka uliopita.
Takwimu za simu za mkononi na usajili wa intaneti zilifikia milioni 21.5 au asilimia 99 ya jumla ya usajili wa mtandao wakati wa robo ya ukaguzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |