• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shilingi ya Kenya imekuwa imara dhidi ya sarafu kuu za dunia wakati wa wiki ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-08-14 19:26:00

    Shilingi ya Kenya imekuwa imara dhidi ya sarafu kuu za dunia wakati wa wiki ya uchaguzi wa mwaka huu ikilinganishwa na uchaguzi mkuu uliopita.

    Takwimu za hivi karibuni kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK) zinaonyesha kwamba shilingi iliongezeka thamani dhidi ya pauni na Euro lakini kidogo imepungua thamani dhidi ya dola wiki ya nyuma.

    Pauni ambayo ilibadilishwa kwa Sh137.33 tarehe 3 Agosti ilipungua kwa shilingi moja na kufikia Sh136.28 kabla ya kushuka hadi Sh135.85 na Sh135.24 tarehe 7 Agosti na 9 kwa mtiririko huo.

    Jana, Pauni ilikuwa inabadilishwa kwa wastani wa sh134.91

    Euro, kwa upande mwingine, ilipungua kutoka Sh123.04 Agosti 3 hadi Sh122.93 tarehe 7 Agosti, usiku wa uchaguzi mkuu wa taifa.

    Kushuka kwa thamani iliendelea baada ya uchaguzi hadi Sh122.46 Agosti 9.

    Shilingi ya Kenya ilishuka kidogo dhidi ya dola ya Marekani wiki iliyopita, kutoka Sh103.85 Agosti 3 hadi Sh103.88 na Sh103.90 mnamo Agosti 7 na 9 kwa mtiririko huo.

    Katika wiki ya mwisho ya uchaguzi wa mwaka 2013, shilingi ilibadilikabadilika dhidi ya sarafu zote kuu.

    Tofauti na miaka ya uchaguzi iliopita ambapo baadhi ya nchi ziliweka vikwazo vya kusafiri, wakati huu Kenya iliweka uwekezaji mkubwa wa kigeni na makampuni kama Volkswagen kurudi baada ya miongo minne miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako