• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya wajumbe wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika yafanyika nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-08-14 20:47:28

    Mazungumzo ya wajumbe wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika yamefanyika mjini Johannesburg Afrika Kusini.

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya habari ya baraza kuu la serikali ya China Bw. Guo Weimin, balozi wa China nchini Afrika Kusini Bw. Lin Songtian, na wajumbe wa vyombo 15 vya habari kutoka China na nchi za Afrika wamehudhuria mazungumzo hayo. Bw. Guo Weimin amependekeza kuwa vyombo vya habari vya pande hizo mbili zinatakiwa kufanya ushirikiano wa kihalisi na kutoa sauti zenye haki na msingi kwa pamoja.

    Mhariri mkuu wa gazeti la The Guardian la Tanzania Bw. Benjamin Mgana amesema anatarajia vyombo vya habari vya China na Tanzania vitaandika ripoti kuhusu Afrika, kuwavutia wawekezaji wa China kuwekeza nchini Tanzania na barani Afrika, na kutoa nafasi nyingi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako