• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-08-15 09:32:26

    Rais John Magufuli wa Tanzania ametangaza kuwa Misri imedhamiria kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama nchini Tanzania.

    Akiongea kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo na rais Al-Sisi wa Misri ambaye yupo ziarani nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema ujenzi wa kiwanda hicho utatoa afueni kubwa kwa wafugaji, watakao kuwa na uhakika wa soko la mifugo yao. Rais Magufuli ameeleza kuwa Misri ina soko kubwa la nyama na nchi hiyo imeiahidi soko kwa Tanzania.

    Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tanzania ni nchi yenye idadi kubwa ya mifugo barani Afrika, lakini haina kiwanda cha kusindika nyama.

    Rais Magufuli amesema mbali na sekta ya ufugaji, Misri pia imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta za afya, elimu, ulinzi na usalama, na kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako