• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo na madhara ya mvua nchini Sierra Leone vyamsikitisha katibu mkuu wa umoja wa mataifa

    (GMT+08:00) 2017-08-15 09:34:25

    Watu 300 wamefariki dunia na wengine elfu mbili wameachwa bila makazi kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Sierra Leone.

    Naibu msemaji wa katibu mkuu Bw Farhan Haq amesema katibu mkuu anasikitishwa na vifo na madhara yaliyosababishwa na mvua hiyo, na kutoa pole kwa serikali na watu wa nchi hiyo kufuatia vifo na uharibifu mkubwa.

    Mvua kubwa ilinyesha jumatatu asubuhi na kusababisha watu wa mji wa Regent karibu na mji wa Freetown kukwama majumbani kwao, kabla ya udongo wa mlima wa karibu kuporomoka kutokana na mvua hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako