• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yataka Umoja wa Mataifa kutoa fedha kwa ajili ya wakimbizi milioni 2 nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-08-15 09:46:57

    Serikali ya Sudan imeutaka Umoja wa Mataifa kutoa fedha kwa ajili ya wakimbizi milioni 2 nchini humo.

    Waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Sudan Bw Idris Suleiman amekutana na mjumbe wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Sudan Bi. Noriko Yoshida, akisisitiza umuhimu wa kuchangia fedha kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi nchini Sudan.

    Bw Suleiman pia amesisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya kambi za wakimbizi na kuwapatia huduma bora. Ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuipatia Sudan msaada wa msingi kwa ajili ya wakimbizi wengi nchini humo, na kuwapatia makazi na uhuru wa kusafiri na kuwasiliana na jamii ya Sudan.

    Bi Noriko Yoshida amesisitiza tena umuhimu wa kazi ya kuandikisha wakimbizi nchini Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako