• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yalenga watalii wa China kukuza ustahimilivu wa utalii

    (GMT+08:00) 2017-08-15 09:52:40

    Serikali ya Kenya inapanga kuvutia watalii zaidi kutoka China ili kuongeza ustahimilivu wa sekta ya utalii.

    Mwenyekiti wa bodi ya utalii ya Kenya Jimi Kariuki amesema, ongezeko la watalii waliotembelea nchini Kenya limezidi asilimia 10. Kenya inapanga kuongeza shughuli za masoko nchini China, ili kukabiliana na kupungua kwa watalii wanaotoka nchi za magharibi.

    Bw. Kariuki pia amesema, Kenya itaendelea kuzingatia soko la China ambalo linazidi kuwa muhimu kwa utalii wa Kenya. Kwa mujibu wa mpango wake, Kenya inatarajia ongezeko la asilimia 35 la watalii wa China mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako