• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yawapokea wakimbizi 70 wanaorejea kutoka DRC

    (GMT+08:00) 2017-08-15 09:57:57

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imeikabidhi Burundi wakimbizi 70 waliokimbia mgogoro uliotokea mwaka 2015 nchini humo, waliokubali kurudi nyumbani kwa hiari.

    Wakimbizi hao 70 kutoka familia 24 wanatoka kambi ya wakimbizi ya Lusenda iliyoko mashariki mwa DRC, na kukaribishwa na serikali ya Burundi katika forodha ya Gatumba.

    Mkimbizi mmoja amesema anaitikia wito wa rais wa Burundi wa kutaka wakimbizi warudi nyumbani.

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani na elimu ya uraia wa Burundi Bw. Terence Ntahiraja aliwakaribisha wakimbizi hao, na kulaani habari za uwongo zilizopo kwenye mtandao wa Internet zinazofanya wakimbizi wakatae kurudi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako