• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanamedali kutua nchini jumanne baada ya kung'aa uingereza

    (GMT+08:00) 2017-08-15 10:13:13
    TIMU ya taifa ya Kenya inatarajiwa kupokelewa kishujaa Jumanne kutoka nchini Uingereza baada ya kumaliza Riadha za Dunia katika nafasi ya pili nyuma ya Marekani.

    Kikosi hicho kimepangiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jumanne asubuhi. Kenya, ambayo ilikuwa inatetea taji ililoshinda nchini Uchina mwaka 2015, ilijizolea medali tano za dhahabu zikiwemo mbili siku ya mwisho ya mashindano kutoka kwa Hellen Obiri (mita 5000) na Elijah Manangoi (mita 1500), fedha mbili na shaba nne.

    Timu hiyo itaongozwa na Rais wa Shirikisho la Riadha la Kenya (AK) Jackson Tuwei na maafisa wengine kutoka shirikisho hilo.

    Baada ya kuwasili, timu hiyo itaelekea katika hoteli ya kifahari ya Weston kwa mapokezi na kiamsha kinywa. Familia ya riadha pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Michezo watakaribisha timu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako