• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakalebela asema Uchaguzi wa TFF haukuwa huru na haki

    (GMT+08:00) 2017-08-15 10:14:36
    Baada ya kuambulia kura tatu katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Fredirick Mwakalebela amesema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki ila anajipanga kugombea tena uchaguzi ujao.

    Mwakalebela alipata kura tatu kwenye uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mkoani Dodoma huku wapiga kura wakimpa ridhaa hiyo, Wallace Karia kura rais kwa kumpa kura 95, akiwaacha kwa mbali sana wapinzani wake Shija Richard, Ally Mayay waliopata kura tisa kila mmoja, Iman Madega kura nane, Mwakalebela 3 na Emmanuel Kimbe kura mmoja.

    Mwakalebela alisisitiza kuwa uchaguzi wa TFF haukuwa huru wala wa haki huku akidai kuwa wajumbe ambao hawakuwa na ruhusa kushiriki uchaguzi huo walipiga kura.

    Aidha, alisema kitendo cha kuvunja kamati ya uchaguzi ilikuwa ni kinyume na katiba ya TFF kwani katiba inasema kamati inapaswa kuwa madarakani katika kipindi cha miaka miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako