• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwizeye ni mwendeshaji baiskeli bora wa Rwanda kwenye Colorado Classic

    (GMT+08:00) 2017-08-15 10:15:15
    Jean Claude Uwizeye alikuwa mwendeshaji bora wa baiskeli katika kikosi cha Team Rwanda baada ya kuorodhesha nambari 47 katika mashindano ya Colorado Classic ilihali Jean Paul René Ukiniwabo alimaliza wa 6 miongoni mwa waendeshaji chipukizi katika mashindano yaliyoandaliwa wikendi iliyopita Marekani.

    Hata hivyo, haikuwa wakati mzuri kwa Didier Munyaneza, aliyekosa kuwahi muda uliowekwa katika hatua ya mwisho ya mashindano ya kitengo cha UCI 2.HC. Mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alitajwa kuwa mwendeshaji aliyevutia kutoka hatua ya kwanza.

    Manuel Senni wa BMC Racing Team, aliyemaliza wa 10 katika hatua ya 4 alitangazwa mshindi kwa jumla hata ingawa hakushinda hatua yoyote katika mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako