• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Diego Costa asema Chelsea hawamtaki tena

  (GMT+08:00) 2017-08-15 10:30:30

  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uispania Diego Costa amesema Chelsea wamekuwa wakimchukulia kama mhalifu na akathibitisha kwamba bado anataka kurejea Atletico Madrid kwani kulingana naye klabu hiyo haimtaki tena.

  Mshambuliaji huyo wa miaka 28 alichezea Chelsea mara ya mwisho fainali ya Kombe la FA mwezi Mei na mwezi Juni alitumiwa ujumbe wa simu na meneja Antonio Conte kumfahamisha kwamba hakuwa kwenye mipango yake ya msimu ulioanza siku chache zilizopita.

  Costa amesema sasa klabu hiyo inamshurutisha kurejea akafanye mazoezi na wachezaji wa akiba na anashangaa ni kwa nini klabu hiyo haitaki kumwachilia aondoke iwapo hawamtaki.

  Costa sasa anasema atafanya uamuzi kwani inambidi afikirie maslahi yake. Kwa maoni yake, yeye amejaribu kufanya kila kitu sawa lakini anataka uamisho kurejea Atletico.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako