• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya askari wa Umoja huo nchini Mali

    (GMT+08:00) 2017-08-15 18:08:25

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres kwa nyakati tofauti wametoa taarifa wakilaani shambulizi dhidi ya askari wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, ambapo askari mmoja kutoka Togo na raia wengi wa Mali waliuawa, na askari mwengine mmoja kujeruhiwa.

    Baraza la Usalama limeitaka serikali ya Mali ifanye uchunguzi mapema, na kuwakamata wahusika wa shambulizi hilo.

    Naye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani tukio hio, na pia amesifu juhudi za nchi tano za Sahel ikiwemo Mali katika juhudi zao za kupambana na ugaidi na kuhimiza amani na maendeleo ya kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako