• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya wajumbe wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika yafanyika nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-08-15 18:31:09

    Mazungumzo ya wajumbe wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika yamefanyika jana huko Johannesburg, Afrika Kusini, na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka vyombo vya habari vya China, Afrika Kusini, Nigeria, na nchi nyingine. Je, hali ya maingiliano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika ikoje? Waandishi wa habari wa Afrika wanaonaje ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari vya China kuhusu Afrika?

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China Bw. Guo Weimin amehutubia mazungumzo hayo akisema, uhusiano kati ya China na Afrika umeingia kiwango kipya, na ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika pia umepata fursa nzuri. Amesema maingiliano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika yana nafasi zaidi ya kuimarika.

    "ikilinganishwa na mahitaji ya maendeleo ya kasi ya uhusiano kati ya China na Afrika, na ushirikiano unaopamba moto kati ya China na Afrika, ufahamu kati ya pande mbili za China na Afrika hautoshi, vyombo vya habari vya China na Afrika vina nafasi kubwa ya kushirikiana. "

    Ametoa mapendekezo matatu kuhusu kuzidisha ushirikiano na maingiliano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika, akisema

    "kwanza, kuimarisha kuaminiana, kuimarisha msingi wa uhusiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika. Pili, kuimarisha ushirikiano na kuhimiza maingiliano kati ya pande hizo mbili kuingia katika kiwango kipya. Tatu, kuhimiza mawasiliano na ushirikiano katika kutoa sauti ya haki na yenye mantiki. "

    Mhariri mkuu wa gazeti la The Sun News la Nigeria Bw. Timothy Olanrewaju amesema, ikitofautishwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi ambavyo vinapenda kutangaza habari mbaya za Afrika, vyombo vya habari vya China vinatoa habari za Afrika kwa kuifikiria Afrika. Anatumai kuwa vyombo vya habari vya China vitapanua shughuli zao barani Afrika.

    "Redio China kimataifa inarusha matangazo ya lugha ya kihausa nchini Nigeria, watu wanapenda kusikiliza habari kuhusu miradi ya ujenzi ya China nchini Nigeria kwa lugha ya kihausa. Natumai Redio China Kimataifa itarusha matangazo mengi zaidi katika nchi za Afrika."

    Mhariri mkuu wa gazeti la Discoverer la Ghana Bw. Elvis Darko amesema China inaweza kufanya mradi wa ripoti wa wiki tatu au nne, ili waandishi wa habari wa Afrika wanaweza kugundua masimulizi kuhusu maisha ya waafrika nchini China.

    "waghana wengi wanaishi na kufanya biashara mjini Guangzhou, lakini je waghana hawajui ndugu wengi wao wako Guangzhou? Wanajua tu wachina wengi wanakuja Ghana kufanya biashara, wanaona Ghana imejaa wachina. Lakini kama waandishi wa habari wa Ghana wanatoa ripoti kuhusu waghana wanaoishi Guangzhou, basi wataelewa wachina kuja Ghana ni hali ya kawaida. "

    Katika mazungumzo hayo, wajumbe kutoka vyombo vya habari vya China wamefanya maingiliano ya ana kwa ana na wenzao wa Afrika, na kutoa matarajio ya mustakabali wa ushirikiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako