• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yakana taarifa kuwa mji muhimu wa mpakani umekaliwa tena na waasi

    (GMT+08:00) 2017-08-15 18:57:20

    Sudan Kusini imekana taarifa zilizotolewa na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar kuwa wanashikilia tena mji wa Pagak ulioko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Ethiopia.

    Msemaji wa kundi la SPLA-IO Dickson Gatluak amesema, taarifa hizo si za kweli, na kwamba vikosi vya serikali ya Sudan Kusini bado vinadhibiti mji huo baada ya mapigano makali yaliyotokea jana. Amesema waasi hao ambao kwa sasa wako sehemu ya kaskazini ya mji wa Pagak walijaribu kuwaondoa askari wa serikali walioko kwenye daraja linalounganisha mji huo na Ethiopia, lakini walishindwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako