• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yawataka Wakenya kujizuia na vurugu za baada ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-08-15 18:57:40

    Serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wa Kenya kuacha vurugu baada ya uchaguzi, kufuatia siku kadhaa za watu kutotembea baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika jumanne iliyopita.

    Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Kenya leo imepongeza taarifa zilizotolewa na waangalizi wa kikanda na kimataifa waliothibitisha kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa uaminifu. Marekani imesema, ina wasiwasi na ripoti kuwa baadhi ya maandamano yamekumbwa na vurugu, na kutoa wito kwa Wakenya kukataa vurugu na kusuluhisha tofauti zao kwa kufuata katiba ya nchi hiyo na utawala wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako