Taakwimu kutoka kwa halamashauri ya kuuza bidhaa za kilimo nje ya nchi (NAEB) zinaonyesha kwamba mauzo ya mwaka jana kipindi sawa na hicho yalikuwa dola milioni 6.1.
Ongezeko la mapato limechangiwa na kuimarika kwa bei kwenye soko la kimataifa ambayo sasa ni dola $3.38 kwa kilo ikilinganishwa na dola $2.43 za mwaka jana.
Aidha chai iliouzwa na Rwanda mwaka huu imeongezeka.
NAEB inasema ilenga kupata dola milioni $94.9 kwa mwaka ifikapo mwaka 2018.
Hadi sasa serikali imegawa zaidi ya miche milioni 13 za chai ili kuongeza uzalishaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |