• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya kulinda wanyama pori Uganda kuhamisha twiga 20 ndani ya hifadhi ya Murchison

    (GMT+08:00) 2017-08-15 19:14:17

    Mamlaka ya kulinda wanyama pori nchini Uganda imeanza kuhamisha twiga 20 ndani ya hifadhi ya Murchison Falls wilaya ya Nwoya.

    Zoezi hilo linalenga kuhamisha wanyama hao kutoka maeneo ya kingo za kaskazini za hifadhi ya Nile Park hadi zile za kusini.

    Msemaji wa malka hiyo Jossy Muhangi, amesema uhamishaji huo wa wiki moja unafanyika kwa ushirikiano wa mamlaka hiyo pamoja na wakfu wa kulinda twiga.

    Hivi karibuni mamlaka hiyo ilipokea misaada ya vifaa vya vya dhamani ya dola 37,500 kuhamisha wanyama hao kutoka kwa wakfuo huo.

    Mwezi juni mwka 2015 mamlaka hiyo ilihamisha twiga 15 kutoka hifadhi ya Murchison Falls hadi ile ya ziwa Mburo ili kukuza utalii magharibi mwa Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako