• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania yateketeza tani 1.6 ya vyakula

    (GMT+08:00) 2017-08-15 19:18:52

    Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA), Kanda ya Ziwa imeteketeza tani 1.6 ya vyakula vya aina mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh2.8 milioni visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.

    Mkaguzi Mwandamizi wa Chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa, Julius Panga amesema leo Jumanne, Agosti 15 kuwa bidhaa zilikamatwa wakati wa ukaguzi wa kushtukiza uliofanyika kwenye maduka ya bidhaa za chakula katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

    Amesema miongoni mwa bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na chumvi aina ya Kaysalt vifungashio vyake vinaonyesha ilitengenezwa kwa ajili ya soko la nchi jirani ya Kenya kwa kuandikwa.

    Bidhaa nyingine ni mafuta ya kupikia ambayo licha ya kuandikwa jina la ufuta kuonyesha yanatokanana mbegu ya ufuta, lakini uchunguzi umebaini yametengenezwa kwa malighafi ya mawese.

    Panga amesema TFDA imelazimika kuyaondoa sokoni na kuyateketeza mafuta hayo baada ya walioingiza bidhaa hiyo kushindwa kutekeleza maelekezo ya kuwasiliana kufanya marekebisho ya jina kutoka ufuta kwenda mawese.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako