• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nahodha wa Cranes aonya dhidi ya utepetevu

    (GMT+08:00) 2017-08-16 10:29:23
    Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Uganda – Uganda Cranes, Benard Muwanga sasa amewaonya wenzake dhidi ya utepetevu baada ya kushinda timu ya Rwanda Amavubi katika mkondo wa kwanza wa mechi ya kufuzu CHAN mwakani.

    Muwanga amesema kuwa ni vizuri kwamba timu yake ilishinda mkondo wa kwanza dhidi ya Rwanda lakini akaonya kuwa kibarua bado kipo kwani chochote chaweza kutokea katika mechi ya marudiano. Kulingana na beki huyo, Uganda lazima ijiandae vyema kuhakikisha ushindi timu hizo zitakapokutana tena wikendi ijayo.

    Vijana wa kocha Moses Basena walijiweka nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuibaniza Amavubi mabao 3-0 jijini kampala wikendi iliyopita na sasa wanahitaji kutoka sare tu au hata kupoteza mechi ya marudiano kwa chini ya mabao 3, ili wafuzu fainali za CHAN zitakazoandaliwa Kenya mwakani.

    Kocha wa Amavubi Antoine Hey amesema kikosi chake kinajiandaa vilivyo kwani bado kuna nafasi ya timu yake kufuzu huku akionya Uganda kuwa Rwanda huenda ikawashangaza itakapocheza mbele ya mashabiki wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako