• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu nane 8 kushiriki mashindano ya ukumbusho ya KAVC

    (GMT+08:00) 2017-08-16 10:30:38
    Vilabu nane vya nyumbani vimethibithisha kushiriki kwao kwa Makala ya 21 ya mashindano ya kimataifa ya voliboli ya NSSF KAVC tarehe 19 na 20 katika uwanja wa Lugogo na Namboole na ule wa chuo kikuu cha Makerere Business school jijini kampala.

    Timu ambazo zimethibitisha kushiriki kwao kwenye mashindano hayo ni ile ya mabingwa watetezi Rwanda Revenue Authority, Chuo kikuu cha Kibungo (UNIK), Kigali Volleyball Club (KVC), Chuo kikuu cha Utalii na teknologia (UTB), Gisagara, Rwanda Energy Group (REG), pamoja na timu ya wanaume na kinadada ya APR.

    Timu za ugenini zitakazoshiriki mashindano hayo ya siku mbili ni kama vile Muzinga na Rukinzo kutoka Burundi, Kenya Administration Police, Prisons, Corporative Bank na Nairobi City Council.

    Idadi kamili ya jumla ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo inatarajiwa kuongezeka hadi 36 kutoka timu 22 zilizoshiriki mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako