• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msemaji wa kundi la Taliban ajeruhiwa vibaya kwenye operesheni ya jeshi la serikali

  (GMT+08:00) 2017-08-16 18:22:05

  Shirika la habari la Afghanistan jana limesema, wapiganaji 25 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa akiwemo msemaji wa kundi hilo Zabihullah Mujahid katika operesheni iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo mkoani Faryab.

  Hivi karibuni, kundi la Taliban limedhibiti kwa muda mfupi sehemu ya Gormach, lakini vikosi vya usalama vya Afghanistan vinaendelea na operesheni ili kudhibiti tena sehemu hiyo.

  Zabihullah Mujahid aliteuliwa kuwa msemaji wa kundi hilo mwezi Januari mwaka 2007, na anashugulikia matangazo kwa eneo la mashariki, kati, na kaskazini mwa Afghanistan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako