• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matayarisho ya maonesho ya biashara ya Rwanda yapamba moto

    (GMT+08:00) 2017-08-16 19:19:28

    Matayarisho kwa ajili ya maonesho ya biashara ya Rwanda mwaka huu yamenoga huku washiriki wengi wakiwa wanajenga vibanda vyao vya maonesho katika uwanja wa maonesho wa Gikondo eneo la Kicukiro.

    Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi Rwanda (PSF),Wizara ya Biashara,Viwanda na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatang'oa nanga tarehe 22 Agosti hadi tarehe 6 Septemba.

    Mkurugenzi wa Shirikisho la Sekta Binafsi Faustin Karasira amesema waonyesha bidhaa 633 wa ndani na kimataifa wamethibitisha kushiriki.

    Serikali ya Rwanda hutumia maonyesho haya ya kila mwaka kuwahimiza wanyarwanda kutumia bidhaa zinazotengezwa nchini,na pia kuwapatia changamoto wenye viwanda kuboresha ubora chini ya mpango wa Made in Rwanda.

    Aidha Karasira ameyahimiza makampuni ya ndani kutumia maonyesho hayo kama fursa sio tu ya kuuza bidhaa zao lakini kama jukwaa la kupanua mitandao na kujenga urafiki wa kibiashara kati yao na wenzao wa kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako