• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kutangazwa India kama kituo cha uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-08-16 19:19:58
    Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na wafanyabiashara wenye viwanda nchini India wameandaa kongamano la kuhamasisha na kukuza uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

    Mkurugenzi Mtendaji wa TIC ,Geoffrey Mwambe amesema lengo la mkutano huo ni kutangaza firsa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

    Kongamano hilo litakalofanyika Agosti 30 litahudhuriwa na wawekezaji wa kampuni kubwa zaidi ya 100 kutoka India ambazo zitasaidia kuitangaza Tanzania.

    Mwambe amesema wawekezaji hao ni kutoka sekta mbalimbali kama vile kilimo,viwanda,usindikaji wa mazao,afya,teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na madawa.

    Mwambe ametoa wito kwa kampuni za Tanzania na sekta binafsi kushiriki kwenye kongamano hilo ili kuweza kuanzisha,kukuza na kuendeleza ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati yao na kampuni za India.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako