• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Moto mkubwa uliotokea soko la Mbeya wateketeza mali za mamilioni ya shilingi

    (GMT+08:00) 2017-08-17 09:36:46

    Moto mkubwa ulitokea usiku wa kuamkia jana na umeteketeza soko kubwa la Mbeya maarufu kama SIDO, pamoja na mali zenye thamani ya mamilioni ya Shilingi za wafanyabiashara wengi wa soko hilo.

    Moto huo ulioanza majira ya saa 3 usiku ulishindwa kudhibitiwa hadi jana asubuhi. Mashuhuda wamesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, huku wakilaumu miundo mbinu mibaya iliyozuia kikosi cha zima moto kwenda kuzima moto kwa wakati. Soko hilo lililojengwa miaka sita iliyopita, likiwa na vioski karibu 4,000 lilikuwa maarufu kwa kuuza bidhaa za aina mbalimbali zikiwemo nguo, bidhaa za kielekroniki za jumla na rejareja.

    Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Ntinika amesema soko hilo lilikuwa kituo cha biashara kilichohusisha wafanyabiashara wa mkoa huo na nchi jirani za Zambia na Malawi. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw Amos Makalla amelaani watu wanaochoma moto kwa makusudi na wahujumu wa uchumi, na kuonya kuwa watakamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako