• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo cha Confucius chazindua kituo cha kwanza cha mtihani wa lugha ya kichina nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:02:56

    Chuo cha Confucius katika chuo kikuu cha Makerere huko Kampala, kimezindua kituo cha kwanza cha mtihani wa lugha ya kichina, kitakachowawezesha watu wa huko kushiriki kwenye mitihani ya kimataifa.

    Kituo hicho kilichozinduliwa na naibu balozi wa China nchini Uganda Bw. Chu Maoming, kitatumiwa kupima uwezo wa lugha ya kichina na uwezo wa kuzungumza kichina kwa ajili ya biashara kwa vijana. Pia kitatoa mtihani wa lugha ya kigeni na mitihani ya kichina katika nchi za nje zilizoidhinishwa.

    Bw. Chu amesema, kituo hicho kitapunguza gharama kwa waganda kwenda Kenya kufanya mitihani ya lugha ya kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako