• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yatoa udhamini kwa wanafunzi 65 wa Ghana kuendeleza masomo nchini China

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:04:00

    Balozi wa China nchini Ghana Bw. Sun Baohong amesema, serikali ya China imetoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi 65 wa Ghana kuendeleza masomo yao katika sekta mbalimbali kwenye vyuo vikuu vya China.

    Bw. Sun amesema hayo kwenye hafla ya kuwaaga wanafunzi hao, huku akieleza kufurahishwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wa Ghana nchini China.

    Bw. Sun amesema China inawapokea wanafunzi wa Ghana tangu mwaka 1960. Hadi sasa wanafunzi 1,006 wa nchi hiyo wamepata udhamini wa masomo unaotolewa na serikali ya China. Hivi sasa wanafunzi 5,516 wa Ghana wanasoma nchini China, idadi ambayo ni ya juu zaidi kati ya wanafunzi wa nchi za Afrika waliokuja kusoma China katika miaka mitatu iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako