• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waihimiza Korea Kaskazini itekeleze wajibu wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:08:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema Korea Kaskazini inatakiwa kutekeleza kwa makini wajibu wa kimataifa, na kushiriki kwenye mazungumzo ili kupunguza hali ya wasiwasi kwenye Peninsula ya Korea.

    Bw Guterres amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2371, linaloeleza wajibu wa amani na usalama unaotakiwa kutekelezwa na Korea Kaskazini.

    Amesisitiza kuwa pande zote husika zinatakiwa kutekeleza kwa makini wajibu wao. Azimio hilo la namba 2371 limezipatia pande zote nafasi za mawasiliano ya kidiplomasia na mazungumzo mapya kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.

    Wakati huo huo, balozi wa Russia nchini Marekani Bw Vassily Nebenzya amezihimiza Marekani na Korea Kusini zipunguze luteka ya pamoja ili kupunguza hali ya wasiwasi kwenye Peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako