• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Iran autaka Umoja wa Ulaya utoe mchango zaidi katika utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:08:34

    Rais Hassan Rouhani ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutoa mchango zaidi katika utekelezaji wa makubaliano ya suala la nyuklia la Iran.

    Akizungumza na balozi wa Austria nchini Iran Bw Stefan Scholz, rais Rouhani amesema Umoja wa Ulaya unatakiwa kutoa mchango zaidi katika utekelezaji wa makubaliano hayo, ambayo yatanufaisha pande zote kwa kuondoa wasiwasi wa nchi za magharibi na kuondoa vikwazo katili dhidi ya Iran.

    Rais Rouhani pia amesisitiza kwamba, Iran inatarajia kuvutia uwekezaji, kuhamisha teknolojia mpya na kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi katika mazingira mapya.

    Habari zinasema, ofisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia Bibi Federica Mogherini, amesema umoja huo utahakikisha makubaliano yanaendelea kutekelezwa, na Umoja wa Ulaya utaendelea kuwasiliana na Iran bila kujali sera za wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako