• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarehe ya uchaguzi ya bodi ya ligi TPLB imewekwa

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:25:27
    Uchaguzi wa Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam. Fomu kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa leo Agosti 17, 2017 kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

    Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watatu kuwakilisha klabu za Ligi (PL), Wajumbe wawili wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL).

    TFF inasema kuwa uchaguzi huo utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za shirikisho hilo toleo la 2013. Wagombea viti mbali mbali kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako