• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji kadhaa wa Uganda Cranes kutoshiriki mechi dhidi ya Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:25:47
    Timu ya soka ya taifa ya Uganda itaondoka leo kuelekea Rwanda tayari kwa mchuano dhidi yake na Amavubi stars kuamua ni nani ataingia CHAN mwakani.

    Lakini timu hiyo inakodolea macho upungufu wa nyota wake baada ya wachezaji kadhaa kujiondoa kambini. Wachezaji Muhamad Shaban na Rashid Toha hawakuwa kwenye kikosi iliyotajwa na kocha Moses Basena na msaidizi wake Fred Kajoba wakati timu hiyo ilifanya mazoezi ya mwisho.

    Mshambuliaji Shaban hajakuwa kikosini tangu timu hiyo irejelee mazoezi mwanzoni mwa wiki hii baada ya kupata jeraha la goti katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Rwanda jijini Kampala.

    Mwenziye Onduparaka vile vile alikosa maandalizi ya mechi ya wikendi baada ya kupatikana na ugonjwa wa kipindupindu.

    Japo kuna wachezaji wa ziada wazuri, Cranes inaonekana kukosa makali yake hasa katika safu ya ulinzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako