• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha Manangoi amezea mate taji Diamond League

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:26:04
    Mwanariadha wa Kenya Elijah Manangoi, sasa anasema anatarajia ushindi katika mashindano yajayo hivi karibuni ya Diamond League baada ya kushinda medali ya Dhahabu katika mashindano ya dunia yaliyokamilika karibuni jijini London.

    Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye pia anahudumu kama afisa wa polisi nchini Kenya, aliwaongoza Wakenya wenzake na kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika mbio za mita 1500 za wanaume na kurejesha ubabe wa Kenya katika mashindano hayo.

    Manangoi kwa sasa anaongoza katika jedwali katika mbio hizo kabla ya mashindano mawili ya mwisho ya msimu huu zitakazoandaliwa katika miji ya Zurich na Brussels.

    Yeye ni Mkenya pekee kati ya mabingwa wa dunia 18 walioalikwa kushiriki mashindano ya Weltklasse Diamond League jijini Zurich Agosti 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako