• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fan Changlong akutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani

    (GMT+08:00) 2017-08-17 16:56:17

    Naibu mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Fan Changlong, leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani Jenerali Joseph F. Dunford.

    Bw. Fan Changlong amesema, China inaamini kuwa mazungumzo ni njia pekee ya kutatua suala la peninsula ya Korea, na si njia ya kijeshi. Amesema pande mbalimbali zinapaswa kujizuia, na kuepuka maneno na vitendo vitakavyozidisha hali ya wasiwasi kwenye peninsula hiyo. China inatumai kushirikiana na Marekani kuhimiza pande mbalimbali kufuata mwelekeo wa pamoja, na kujitahidi kutatua suala la nyuklia la Korea kaskazini na kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea.

    Kwa upande wake, Jenerali Dunford amesema, Marekani inapenda kushirikiana na China kutekeleza makubaliano ya viongozi wa nchi hizo mbili, na kufanya ushirikiano na maingiliano ya sekta mbalimbali kati ya majeshi ya nchi hizo mbili kwa wazi na kitaaluma, pia kujenga njia ya mawasiliano ya karibu zaidi, kuzidisha uaminifu, kupunguza mkwaruzano, kudhibiti hatari, na kuhimiza maendeleo yenye utulivu ya uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako