• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu washauri utumizi wa treni ,baiskeli au kutembea kukabiliana na msongamano jijini

    (GMT+08:00) 2017-08-17 18:27:10

    Wataalamu wa masuala ya miradi ya maendeleo wametoa ushauri wa utumiaji wa treni ,baiskeli au hata kutembea hadi jijini kuwa njia mbadala za kupunguza msongamano kati kati mwa jiji la Nairobi.

    Wakiongea kwenye kumbi za mijadala ya biashara na maendeleo ,wamesema mipango hii itafanikisha azimio la baraza la jiji la Nairobi kurahisisha biashara na kutoa nafasi katika jiji.

    Pendekezo hili linajiri kufuatia takwimu za hivi punde za benki kuu ya dunia zilizoonyesha kwamba asilimia 26 ya wakenya wanaishi katika sehemu za miji kutafuta fursa za kazi.

    Wataalamu hao wamelitaka baraza la jiji kutengeneza njia maalaum za baiskeli na zile za kutembea kwa miguu.

    Mbinu hii imefanikiwa pakubwa katika baadhi ya miji ya nchi mbali mbali za ulaya.

    Msongamano wa magari na watu katika miji umepelekea kupotea kwa masaa mengi ya kazi na mapumziko kila mwaka na hivyo kuchokesha watu na kuwapa hasara ya matumizi mafuta ya magari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako