• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Unga wa mahindi wa bei nafuu waadimika tena madukani

    (GMT+08:00) 2017-08-17 18:28:18

    Unga wa sima ama ugali wa bei nafuu umeanza kuadimika tena madukani wiki hii .

    Muungano wa wasagaji nchini Kenya CMA umearifu wakenya kuondoa hofu kwani wana hifadhi ya kutosha.

    CMA wamesema kasoro hiyo imetokana na kusitishwa kwa shughuli za usagaji wakati wa uchaguzi mkuu na pia kutokana na ongezeko kubwa la wateja walionunua unga kwa viwango vikubwa ili kuhifadhi makwao kwa hofu ya kutofunguliwa maduka baada ya uchaguzi.

    Paloma Fernandez mkurugenzi mkuu wa CMA ameahidi kuwa unga huo utapatikana kwa viwango vya kutosha wiki hii baada ya shughuli za biashara kuregea hali ya kawaida.

    Serikali ilitoa ruzuku na kupunguza bei hadi shilingi 90 kwa unga wa ugali wa kilo 2 baada ya kununua mahindi kutoka nje ya nchi kufuatia kukosekana kabisa kwa unga wa mahindi nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako