• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani

    (GMT+08:00) 2017-08-17 19:06:49

    Mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni rais wa China Xi Jinping leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti mnadhimu wa jeshi la Marekani Jenerali Joseph F. Dunford.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili ni sehemu muhimu kwa uhusiano kati ya nchi hizo, na kwamba kuhimiza maendeleo ya kiujenzi ya uhusiano ya kijeshi kutatuliza maendeleo ya kina ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Amesema nchi hizo zinatilia maanani kuhimiza maingiliano na ushirikiano kati ya majeshi yao.

    Kwa upande wake, Jenerali Dunford amesema, Marekani inapenda kushirikiana na China kutekeleza makubaliano ya viongozi wa nchi hizo mbili, na kufanya ushirikiano na maingiliano ya sekta mbalimbali kati ya majeshi ya nchi hizo mbili kwa wazi na kitaaluma. Pia kujenga njia ya mawasiliano ya karibu zaidi, kuzidisha uaminifu, kupunguza mkwaruzano, kudhibiti hatari, na kuhimiza maendeleo yenye utulivu ya uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako