• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawili wakamatwa kuhusiana na shambulizi la kigaidi Barcelona

    (GMT+08:00) 2017-08-18 09:56:51

    Watu wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na shambulizi la kigaidi nchini Hispania, baada ya gari moja jeupe kuparamia watu katika eneo maarufu la kitalii la Las Ramblas huko Barcelona.

    Watu 13 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya mia moja wamejeruhiwa katika shambulizi hilo, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.

    Kwa mujibu wa polisi ya huko, dereva wa gari hilo si mmoja wa watu hao wawili waliokamatwa, na mpaka sasa hajulikani alipo.

    Waziri mkuu wa Hispania Bw. Mariano Rajoy amelaani shambulizi hilo na kutangaza siku tatu za maombolezo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres pia amelaani vikali shambulizi hilo.

    Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako