• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Tanzania wazuia wafanya biashara kujenga vibanda vya biashara katika soko la Sido

    (GMT+08:00) 2017-08-18 18:04:08

    Wafanyabiashara katika soko la Sido nchini Tanzania walionekana wamejikusanya kwenye vikundi baada ya kuzuiliwa kujenga tena vibanda vyao vya biashara katika soko hilo ambalo liliteketea kwa moto. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa soko hilo Charles Syuonga,hivi sasa wanasubiria wajumbe wa bodi ya soko hilo kutoa mwelekeo kwa wafanyabiashara. Hadi kufikia sasa Polisi bado wameweka ulinzi mkali kwenye soko hilo wakiwa na lengo la kuwazuia wafanyabiashara kujenga vibanda vyao vya kibiashara.Hata hivyo kamanda wa polisi katika mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amesema wanafuata agizo la serikali linalowataka wafanyabiashara hao kupata kibali kabla ya kuanza ujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako