Tawi la kwanza la Benki ya Maendeleo ya BRICS limefunguliwa hivi karibuni nchini Afrika Kusini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying ametoa pongezi kwa ufunguzi wa tawi hilo, na kusema China itatoa mchango kuzisaidia nchi za Afrika kujiendeleza.
Msemaji huyu amesema Benki ya Maendeleo ya BRICS ni sehemu muhimu ya utaratibu wa ushirikiano kati ya Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, na injini ya maendeleo ya pamoja ya nchi hizo. imeongeza nguvu mpya kwenye ushirikiano wa kusini na kusini.
China itaandaa mkutano wa 9 wa viongozi wa nchi za BRICS mjini Xiamen tarehe 3 hadi tarehe 5 Septemba, na inatarajia kushirikiana na pande mbalimbali kuuhimiza mkutano huo kupata mafanikio mengi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |