• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China watoa salamu za rambirambi kutokana na shambulizi la kigaidi nchini Hispania

    (GMT+08:00) 2017-08-18 18:45:58

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing ametoa salamu za rambirambi kwa mfalme wa Hispania Felipe VI kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea mjini Bacelona.

    Rais Xi amesema, China inapinga aina yoyote ya ugaidi, na inapenda kushirikiana na Hispania na jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi na kulinda amani na utulivu wa dunia.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Hispania Mariano Rajoy kutokana na tukio hilo. Amesema, China inaunga mkono Hispania juhudi za kupambana na ugaidi na kulinda usalama wa taifa, na inapenda kushirikiana na Hispania kutoa mchango katika kuhimiza amani na usalama wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako