• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi 99 wa China wa kulinda amani wafunga safari ya kwenda Sudan

    (GMT+08:00) 2017-08-19 17:54:58
    Wanajeshi 99 wa China jana wamefunga safari ya kwenda Sudan, na watafanya kazi za kulinda amani katika sehemu ya Darfur nchini humo. Kabla ya hapo wanajeshi 41 wamesha pelekwa huko Darfur.

    Mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, kwa mara ya kwanza, China itatuma kikundi cha wanajeshi 140 wa helikopta kushiriki kwenye kazi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa barani Afrika.

    Hadi sasa China imewatuma wanajeshi elfu 33 kushiriki kwenye juhudi za Umoja wa Mataifa za kulinda amani duniani kote. Idadi hiyo ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi wanachama wengine wanne wa kudumu wa Baraza la Usalama la umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako