• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wanne wauawa katika shambulizi la mzinga kwenye maonyesho ya kimataifa ya Damascus

  (GMT+08:00) 2017-08-21 09:50:38

  Watu wanne wameuawa na wengine kumi wamejeruhiwa katika shambulizi la mizinga lililotokea kwenye maonyesho ya kimataifa ya Damascus, Syria.

  Habari zinasema mzinga mmoja ulianguka kwenye jumba la maonyesho hayo na kulipuka kwenye lango moja. Majeruhi walikimbizwa hospitali, wengi wao wamejeruhiwa vibaya.

  Ubalozi wa China nchini Syria umethibitisha kuwa mashirika zaidi ya 20 ya China yameshiriki kwenye maonyesho hayo, lakini hadi sasa hakuna habari kuhusu raia wa China kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

  Maonyesho hayo ya siku kumi yaliyofunguliwa tarehe 17 mwezi huu, yameshirikisha mashirika zaidi ya 1,600 kutoka nchi 43 duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako