• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 499 wafariki kutokana na maporomoko ya udongo Sierra Leone

  (GMT+08:00) 2017-08-21 10:04:45

   

  Habari kutoka Sierra Leone zinasema, hadi sasa mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yaliyotokea huko Freetown, na sehemu za jirani yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 499.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu waliofariki ni pamoja na wanaume 162, wanawake 163 na watoto 156, na hali halisi za wengine 18 bado hazijatangazwa.

  Takwimu za mwanzo za Shirika la msalaba mwekundu zimeonesha kuwa, maafa hayo yatasababisha watu zaidi ya 3,000 kukimbia makazi yao.

  Serikali ya China imeamua kutoa msaada wa dola za kimarekani milioni 1 kwa nchi hiyo, na kampuni za China zilizoko nchini humo pia zimetoa msaada wa fedha, chakula, maji ya kunywa, dawa na nguo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako