• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza uzinduzi wa kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-08-21 18:44:52

    Hafla ya uzinduzi wa kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China na utoaji wa ripoti ya utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 nchini China imefanyika hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping ametoa pongezi kwa uzinduzi huo na kusema serikali yake imetunga mpango wa kutekeleza ajenda hiyo kwa uwiano katika sekta za uchumi, jamii na mazingira, na imepata mafanikio. Amesema China itashikilia kutekeleza ajenda hiyo, na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya nchi yenye sifa nzuri, ufanisi mkubwa na usawa.

    Rais Xi pia amesema anatarajia kituo hicho kitatoa mchango kwa utafiti wa mawazo ya maendeleo, kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa kwenye kazi ya maendeleo, na kuhimiza utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako