• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto zaidi 4000 wamepoteza makazi kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2017-08-22 10:09:04

    Naibu waziri wa habari na wawasiliano wa Sierra Leone Bw Cornelius Deveax amesema watoto zaidi 4000 wamepoteza makazi baada ya mafuriko na maporomoko ya udongo kutoka karibu na mji mkuu Freetown.

    Amesema baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yamewahifadhi baadhi ya watoto na watoto yatima kutokana na maafa hayo.

    Habari pia zinasema shirika la afya la Kimataifa WHO limetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea magonjwa baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababisha vifo karibu watu 500 nchini Sierra Leone.

    WHO inasema kkutokana na kuharibika kwa vifaa vya maji na usafi, wakazi wa maeneo yaliyoathiria ni rahisi kukumbwa na magonjwa ya kuambikiza, yakiwemo Malaria, homa ya matumbo na kipindupindu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako