• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Japan kuheshimu juhudi ya China katika kulinda amani na utulivu wa bahari ya kusini ya China

    (GMT+08:00) 2017-08-22 19:04:01

    Waziri wa mambo ya nje wa Japan Bw. Taro Kono ametoa wito wa kufanya utawala kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha uhuru wa usafiri.

    Waziri huyo amesema hayo katika mkutano wa kimataifa wa ngazi ya mawaziri kuhusu maendeleo ya Afrika (TICAD) alipokuwa akizungumzia kuhusu China kuimarisha shughuli za bahari.

    Akizungumzia kauli hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bibi Hua Chunying amesema lengo la mkutano wa TICAD ni kuiunga mkono Afrika kutimiza amani na maendeleo, na kama habari hiyo ni kweli, Japan ina lengo jingine la kuandaa mkutano huo.

    Amesema China inaitaka Japan kutekeleza kihalisi ahadi ya kuboresha uhusiano kati yake na China, kuheshimu juhudi ya China katika kulinda amani na utulivu wa bahari ya kusini ya China, na kufanya mambo ya kiujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako