• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNICEF yaeleza wasiwasi wake wa kuwatumia watoto wa kike kama mabomu ya kibinadamu

  (GMT+08:00) 2017-08-22 19:21:48

  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema lina wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ukatili na matumizi mabaya ya watoto, hususan wa kike, kama kile kinachoitwa "mabomu ya kibinadamu" katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

  Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo mjini Geneva imesema, tangu mwezi Januari mwaka huu, watoto 83 wametumiwa kama mabomu ya kibinadamu, 55 kati yao ni wasichana wenye umri wa chini ya miaka 15, huku 27 ni watoto wa kiume, na mmoja alikuwa ni mtoto mchanga aliyebebwa na mtoto wa kike.

  Taarifa hiyo imesema, matumizi ya watoto katika mashambulizi kama hayo yana athari kubwa kwa watoto ambao wameachiwa huru, wameokolewa, au wametoroka kutoka kundi la Boko Haram.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako