• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha ushirikiano kwenye eneo la raslimali watu kati yake na Afrika

    (GMT+08:00) 2017-08-23 09:35:59

    China itaendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika kwenye eneo la raslimali watu kwa kuimarisha kuzipatia nchi za Afrika ujuzi na teknolojia.

    Konsela mkuu wa ubalozi wa China nchini Ethiopia Bw Liu Tao amesema tangu mwaka 2000, China imetuma zaidi ya wataalamu 2,000 wa kilimo na zaidi ya wataalamu 7,000 wa afya barani Afrika, na imetoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ya elfu 80 wa Afrika kutoka zaidi ya nchi 70.

    China pia imesema katika muda wa miaka mitatu ijayo, itatoa mafunzo ya kitaalamu kwa watu elfu 20 kutoka Afrika, na itatoa nafasi elfu 40 za mafunzo na udhamini wa masomo kwa wanafunzi zaidi ya elfu 30 kutoka nchi za Afrika.

    Wanafunzi wanaopata mafunzo nchini China wamekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii wanaporudi katika nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako